Chama cha Viziwi Tanzania - CHAVITA- tawi la Morogoro kimetishia kuhamasisha wanachama wake wasijitokeze katika kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi ujao kwa madai kuupuzwa kwa haki zao mbalimbali.
Akizungumza kuhusiana na kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea za Udiwani, Ubunge na Urais ,Katibu wa CHAVITA Mkoa wa Morogoro, HENRY MTASIWA amesema wanafikiria kutoshiriki katika uchaguzi huo kutokana na kutoshirikishwa katika kampeni hizo.
Amesema tayari walishawasilina na viongozi wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi wa mwaka huu, kuhusu kuwekwa kwa wakalimani katika mikutano ya kampeni ili jamii ya viziwi waelewe sera za kila mgombea lakini hadi sasa wamepuuzwa.
Katibu huyo amesema kuwa licha ya kuwasilina na viongozi wa vyama hivyo, pia CHAVITA iliwasilina na Tume ya Uchaguzi kuhusiana na suala hilo la kuwekewa wakalimani lakini mpaka sasa jambo hilo limepuuzwa .
0 comments:
Post a Comment