Moto uliozuka katika mlima wa meru siku tatu zilzopita bado
umeendelea kuwaka huku jitihada
mbalimbali za udhibiti zikiendelea kwa ushirikiano baina ya shirika la
hifadhi za taifa nchini na wananchi wa vijiji vya jirani.
Akizungumza mazingira ya moto huo katika eneo la tukio meneja mawasiliano wa tanapa
pascal shelutete anasema chanzo
cha moto huo ni shughuli za binadamu wakiwemo watu wanaowasha moto kwa
ajili ya kurina asali.
Hata hivyo tanapa inawatoa hofu wananchi wa arusha na maeneo
ya jirani kuhusu taarifa zilizoenezwa na
baadhi ya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuwa moto huo umesababishwa na mlipuko
wa Volcano.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la arumeru mashariki joshua
nasari aliyefika eneo la tukio kushirikiana na wananchi kudhibiti
moto huo Anatoa wito kwa wananchi kuendeela kujitokeza na nguvu kuongezwa ili kunusuru rasilimali
hiyo muhimu kwa maisha ya wananchi na utalii.
Mlima Meru ni mlima wa pili kwa urefu Tanzania. Mlima huu
uko ndani ya hifadhi ya Arusha (Arusha National Park).
Ni sehemu ya aina yake
kwa wale wanaopenda kuangalia ndege wa aina mbali mbali pamoja na wanyama pori
wengine walio katika eneo hilo.
Kilele cha mlima Meru hufikiwa kwa kukatisha
kati ya mabonde ambayo huto picha ya kuvutia ya vinu vya Volkano vilivyoko futi
kadhaa chini ya njia hiyo ya hatari na ya kuteleza. Muda mzuri wa kupanda mlima
huu na mnamo kati ya mwezi Oktoba na Febryary, pamoja na Juni mpaka Septemba
ambapo panakua ni baridi zaidi.
0 comments:
Post a Comment