Image
Image

Mahakama ya mwachia huru Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha.

Mahakama ya Ilala Dar es salaam imemwachia huru mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma za ubakaji dhidi yake.
Akizungumza kwa njia ya simu na Tambarare Halisi Mbasha amesema mahakama imefikia hatua hiyo baada ya kugundua hana kosa lolote,na anamshukuru Mungu kwa Ushindi wake huo.
“kwa kweli Mungu ni mkubwaamesikia kilio changu, na hatimae leo nimeachiwa huru, nimepitia kipindi kigumu sana kwa kweli, nawashukuru sana kwa kuniombea, kunifariji na kwa kunisapoti kwa kipindi chote nilichokuwa na matatizo”, alisema Mbasha.
Emanuel Mbasha alikumbwa na tuhuma hizo mnamo mwezi Julai mwaka 2014, na kesi yake kuendeshwa katika mahakama ya Wilaya Ilala ambapo leo ndio imetoa hukumu ya kesi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment