Mratibu wa Taifa wa THRC, Onesmo Olengurumwa(Kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa.
MTANDAO wa watetezi wa
haki za binadamu nchini THRDC umevitaka vyombo vya habari kuripoti habari kwa
kuzingatia taaluma yao na kuwataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwatafutia
namna waandishi wao wasiongozane na vyama vya siasa kwani wanaminywa katika
uandishi wao.
Akizungumza na waandishi
wa habari mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini Bwana.Onesmo
Olenguruwa amesema baadhi ya vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiripoti
habari zao kwa chama kikuu tu pasipo kuripoti habari kama taaluma yao inavyo
wataka jambo ambalo si jema katika taaluma na huenda likasababisha machafuko
katika taifa.
Amesema kuwa walichokiona
ni namna ambavyo baadhi ya vyama vimekuwa vikiwatumia waandishi wa habari
kuripoti habari za kweli kutoka kwenye vyama vyao bila kuripoti habari hizo
kama zinavyo hitajika kuripotiwa na hivyo kuacha mambo mengine ambayo yangeweza
kujenga.
Ngurumwa ametumia nafasi
hiyo kuvilaani baadhi ya vyombo vyenye mitazamo ya kiitikadi ikiwemo vyombo vya umma
jambo linalorudisha nyuma Demokrasia na kuwanyima fursa wananchi ya kufanya
maamuzi sahihi kwa kuchangua kiongozi wanayemtaka.
Amesema endapo viombo vya
habari vitatumia kalamu yao kwa weledi na taaluma wataweza kufanya watanzania waelewe
kile kitakachojiri kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa kuchagua
Wabunge,Diwani na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Aidha ameiasa mamlaka ya
Mawasiliano nchini TCRA kuhakikisha kuwa inawachukulia hatu wale wote ambao
wataonekana kushabikia upande mmoja wa shilingi katika uchaguzi huu kama ilivyo
fanya siku za usoni kwa baadhi ya viombo vya habari kuegemea upande mmoja.
Ngumwa amevipongeza
vyombo vya habari ambavyo vimeonesha taswira nzuri kwa kipindi hiki cha kampeni
kwa kuripoti habari pasipo kuegemea upande wowote wa shilingi na kuviasa
kuendelea hivyo hivyo hadi mwisho wa Uchaguzi huu.
0 comments:
Post a Comment