Picha ikionesha treni ya reli ya kati.
Abiria waliokuwa wakisafiri kwa Treni ya Reli ya Kati
kutokea jijini Dar es salaam kuelekea Morogoro,Dodoma,Tabora,Mwanza na Kigoma wamekwama na kushindwa
kuendelea na safari yao hivi leo.
Inaelezwa kuwa safari hiyo tangia jana imeshishindikana hadi
leo hii kwa kile kinacho elezwa kuwa baada ya Treni hiyo kufika Pugu jijini Dar
es Salaam kuna ajali ambayo imetokea hivyo safari haiendelei.
Abiria waliokuwamo humo wameendelea kuitupia lawama na
mamlaka husika juu ya usafiri huo ikizingatiwa wana watoto na hata kipato
walicho nacho hakitoshi kwani watakitumia njiani kabla ya safari.
Abiria hao wanasema kuwa kwa hali ilivyo ya mlipuko wa
kipindu pindu kwenye treni hiyo si salama kwao kwani hata vyoo vinaogofya
maisha yao kwa kuwa vinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa mda wowote hali
ambayo si nzuri.
Wameomba juhudi za mapema zifanyike ili wajue hati ya safari
yao kuliko kukaa njiani humo bila mafanikio yeyote yale huku wakielezwa kuna
ajali imetokea inayo zuia wao kuendelea na Safari.
Taarifa Kamili.
Taarifa Kamili.
Abiria
waliokuwa wakisafiri kwa gari moshi kupitia reli ya kati wamekwama kwa saa kumi
na sita katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku
wakilalamikia kutelekezwa na shirika la reli Tanzania katika sehemu ambayo
hakuna huduma muhimu za kijamii.
Baada ya
Tambarare Halisi kupata fununu kuhusu
kukwama kwa gari moshi hilo lenye jumla ya mabehewa 12 kuelekea mikoa
mbalimbali,tulifika katika eneo la pugu na kukuta baadhi ya abiria wakiwa
wamechoka kutoka na njaa huku wengine wakiwa wamelala,na wengine wakipaza sauti
zao kulalamikia kitendo cha kutelekezwa katika eneo hilo huku viongozi wahusika
wa treni hiyo wakikimbia.
Baadhi
ya wagonjwa nao wakatupa lawama kwa shirika la reli Tanzania kwa kuwatelekeza
huku wakihofia maisha yao na maisha ya watoto katika eneo hilo.
Meneja
uhusiano wa shirika la reli Tanzania ambaye licha ya kukiri kuwepo kwa ajali ya
Treni ya mizigo kati ya Soga na Pugu, alishindwa kueleza vizuri sababu
zilizowafanya viongozi walikuwa wakisafiri na treni hiyo akiwemo mkuu wa kituo
cha Pugu kukimbia na kufunga ofisi.
Fuatilia Habari zetu kujua zaidi,Like Page yetu kuwa wakanza
kusoma habari.
0 comments:
Post a Comment