MKALI wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Nasib Abdul ‘Diamond
Platinumz’ na wakali wa Afro Pop kutoka Kenya wanaounda kundi la Sauti
Sol, wamefanya onyesho kabambe katika hitimisho la Tamasha la 2015
Content Showcase Extravaganza, lililofanyika visiwa vya Mauritius.
Onyesho hilo lililofanyika katika hitimisho la wiki ya furaha,
burudani na mafanikio makubwa kwa Kampuni ya MultiChoice Africa,
liliwakutanisha waandishi zaidi ya 90 kutoka kote Afrika, wasanii
mashuhuri na watu maarufu waliokutana katika visiwa hivyo.
Katika onyesho hilo Diamond, Sauti Sol na Mnigeria ambaye ndiye wa
kwanza kufanyakazi chini ya usimamizi wa VP Records, walionyesha uwezo
mkubwa wa kulitawala jukwaa na kufanya ambavyo mashabiki wao walitarajia
kutoka kwao.
Hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo lililokuwa na dhumuni la kuonyesha
maudhui yaliyopo kwenye ving’amuzi vya DStv lililohitimishwa juzi,
lilifanyika kwenye hoteli ya Outrigger Resort ambapo msanii kutoka
Nigeria, Mr Flava alitumbuiza huku mastaa wengine akiwemo, Genevieve
Nnaji, Ramsey Nuoah, Rita Dominic na Desmond Elliot wakimshuhudia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment