MSANII wa hip hop nchini Marekani, Jayceon Taylor
‘The Game’, amesema anamtafuta mtu aliyevunja vioo vya gari lake aina ya
Lamborghini.
Mtandao wa TMZ umeeleza kwamba, msanii huyo
alivamiwa na watu wasiojulikana na kuvunja vioo vya gari hilo likiwa
limeegeshwa eneo la barabara.
Kupitia akaunti ya mtandao wa Instagram, msanii huyo
amesema anamtafuta mtu aliyehusika na tukio hilo ili akabiliane naye.
“Kama kuna mtu anamjua mhusika wa tukio hilo
anijulishe, nitatoa zawadi nono, ninaamini atapatika,” alisema The Game kwa
hasira.


0 comments:
Post a Comment