ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Dk Willbrod Slaa amesema hana haja ya kuwazungumzia viongozi
wanaomaliza muda wao madarakani, badala yake anamlenga kiongozi
atakayekuwa rais wa nchi kwa miaka mitano ijayo.
Dk. Slaa alisema hayo Dar es Salaam jana katika mahojiano maalum na mwandishi mkongwe, Tido Mhando wa televisheni ya Azam.
Akijibu swali kuhusu kwa nini anamzungumzia tu mgombea urais wa
Chadema anayewakilisha Ukawa, Edward Lowassa badala ya kuzungumzia
ufisadi kama mfumo mzima wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
Slaa alisema:
“Tido, nilielezea juu ya Serikali ya CCM akiwamo Rais Kikwete
(Jakaya) ndiyo iliyomlea Lowassa (Edward)… John Mnyika bungeni aliwahi
kusema Kikwete ni dhaifu hilo halina utata, lakini hivi sasa
hatumzungumzii Kikwete kwa kuwa anaondoka na ameshaagwa.
“Tunapoteza muda kwa mtu ambaye kesho hayupo, hapa tunamzungumzia
mtu ambaye tutakuwa naye kama rais wetu kwa miaka mitano ijayo,”alisema
Dk. Slaa.
Kuhusu kuwataja mafisadi wengine, katibu mkuu huyo wa zamani wa
Chadema alisema hajawahi kupata kigugumizi cha kuwataja mafisadi na
kudai kwamba aliwahi kuwataja baadhi ya viongozi kwa ufisadi ndani ya
ofisi ya Ikulu kwenye mikutano ya hadhara na hakukamatwa kwa kuwa
alifanya utafiti.
“Nazungumzia hawa kwa kuwa madhara (impact) yao ni kubwa kuliko hao
wengine lakini tutaendelea kuwapigia kelele kama ilivyo kwa watumishi
wengine hadi wakaondolewa kwa hiyo tulikwenda kuwataja watu na
sikumung’unya maneno,”alisema.
Katika mahojiano hayo maalum, Dk. Slaa alikiri kwamba alihama
nyumbani kwake kwa muda kutokana na vitisho dhidi yake na kudai kuwa
alitoa taarifa ya kupatiwa ulinzi kuhakikisha usalama wake.
“Ni kweli na ndiyo maana sikuficha kama nilikuwa Serena hata hivyo
sikuona kuwa ni kitu cha ajabu na mbona watu hawajiulizi kwamba 2010
kipindi nagombea urais nililala Serena kwa nini leo liwe jambo la ajabu
wakati hii si mara yangu ya kwanza,”alisema Dk. Slaa.
Home
News
Dk. Slaa ajichanganya yupi anamlenga*Asema hana haja ya kuzungumzia viongozi wanao maliza muda wao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment