Image
Image

ACT:Asilimia 94 ya Watanzania hawanufaiki na mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo ANNA MGHWIRA amesema,asilimia 94  ya Watanzania hawanufaiki na mifuko ya Hifadhi ya Jamii,na hivyo wanafika uzeeni wakiwa hawana msaada wowote.
Amesema iwapo  ACT  Wazalendo itaingia madarakani,mifuko hiyo ni kipaummbele cha kwanza,kumwezesha mwananchi kuwa na uhakika awapo mzee.
Ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeini, kwenye  viwanja vya Town School Manispaa ya Tabora.
Mgombea huyo wa Urais  amesema , iwapo chama cha ACT Wazalendo kitapewa ridhaa ya kushika madaraka ya nchi, Serikali yake itawawezesha wananchi walio katika ajira ndogo ndogo kujiwekea akiba ambayo itakuwa msaada kwa maisha yao ya baadaye.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa Urais  wa ACT Wazalendo,   AHAMAD YUSUPH amesema , kila mkoa una matatizo yake ya uchumi na hivyo Mkoa wa Tabora una tatizo la kutonufaika na kilimo cha tumbaku,  na iwapo ACT Wazalendo  kikiingia madarakani ujenzi wa kiwanda cha kusindika tumbaku kitapewa kipaumbele.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment