akihutubia maelfu ya wananchi
mjini bukoba Mheshimiwa Mkapa amesema ili uchumi wa watanzania uimarike ni
lazima mahusiano ya nchi hii na nchi jirani yaboreshwe pamoja na kuweka ulinzi
katika mipaka ya kimataifa ili kuhakikisha kusiwepo
machafuko yanayoweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama
cha mapinduzi mkoa wa Kagera Costansia Buhiye amewataka wananchi kukumbuka
historia ya nchi hii ilikotoka na inakokwenda huku akiwataka kutowaunga mkono
viongozi wanaodandia vyama vya siasa kwa uchu wa madaka na kuwaomba
wananchi kuchagua viongozi kutoka ndani ya chama cha mapinduzi kwakuwa wao ndio
wanauwezo wakusimamia shughuli za maendeleo ya wananchi na kuhakikisha taifa linapiga
hatua zaidi kiuchumi.
nao baadhi ya
wagombea wanafasi za ubukonge katika mkoa huo wamewaomba wananchi kuwachagua
ili waweze kushirikina na mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho John Pombe Magufuri
katika kusuma gurudumu la maendeleo ya wananchi wa mkoa huo na taifa kwa
ujumla.


0 comments:
Post a Comment