FDLR moja kati ya makundi ya kivita, limekuwa likidhoofisha
usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tangu mwaka 1994.
Ushirikiano huo unakuja licha ya uwepo wa jeshi la umoja wa
mataifa MONUSCO, jeshi ambalo pia limewekwa kwa lengo la kutuliza hali ya mambo
nchini Congo.
Kundi la waasi wa Rwanda FDLR limekuwa tishio la muda mrefu
mashariki mwa DRC tangu mauaji ya kimbali ya mwaka 1994 nchini humu yamalizike.
Jitihada mbalimbali zimekuwa zikiundwa ili kulitokomeza
kijeshi kundi hilo cha ajabu bado linaendelea kujigamba, huku wahanga wakuu
zaidi wakiwa ni wanawake wa DRC pamoja na wakazi wa maeneo ambayo FDLR limekita
mizizi.
Moja kati ya jitihada hizo ni uwepo wa makundi mbalimbali ya
umoja wa mataifa MONUSCO mashariki mwa nchi hiyo, jeshi ambalo hadi leo
halijafanikiwa kuwaondosha milele waasi hao.
Ni kwa mantiki hiyo, mawaziri wa DRC na Rwanda wakiambatana
na wakuu wao majeshi, wamekutana jijini Kigali na kutiliana saini za
ushirikiano wa kuling’oa kundi hilo kijeshi ili kupunguza vikundi vya majeshi
mashariki mwa DRC.
Waziri wa ulinzi wa Rwanda James Kabarebe amesema mkutano
huo pia utaangazia changamoto za usalama zinazokabili nchi hizi mbili.
Waziri huyo amesema mwezi Januari mwaka 2009 mataifa haya
yaliungana pamoja na na kufanikiwa kuvunja nguvu za
makundi mbalimbali mashariki mwa nchi jirani ya DRC.
Msemaji wa jeshi la Rwanda Brigedia Josefu Nzabamwita,
ameviambia vyombo vya habari kwamba, muungano huu utalig’oa kundi la waasi wa
Rwanda FDLR milele.
Hii si mara ya kwanza majeshi ya ulinzi ya DRC na yale ya
Rwanda yashirikiane ili kuling’oa kundi hilo, kwani mwaka 2009 mataifa haya
yaliunda shirika liitwalo umoja wetu lililokuwa na malengo ya kudhoofisha
vikundi mbalimbali vya kivita mashariki mwa Jamhuri ya Congo hasa FDLR na CNDP.
Baadaye umoja huo ulivunjika baada ya serikali ya DRC
kuishutumu Rwanda kwa kufadhili kundi la waasi wa jeshi la DR Congo
lililokuwa likiongozwa na muasi Raulent Nkunda, kundi la CNDP.
0 comments:
Post a Comment