Baadhi ya Watanzania walioko Hijja na ambao wamenusurika na maafa ya msongamano wa watu huko Mina jana. Kulia nia Bw. Yahaya Sameja, kushoto ni mwigizaji mchekeshaji Bw. Amri Athumani al maarufu kama King Majuto. Wa katikati jina lake halikuweza kupatikana.
Bismilah Rahman RaheemAssalaam alaykum warahmatullahi wa barakaatuhu.Taarifa hii inahusu tukio lilitokea jana Mina Saudi Arabiawakati mahujaji wakielekea kwenye Jamaraat , palitokea msongamano mkubwa (stampede) na kupelekea mahujaji zaidi ya 700 kufariki na mamia kadhaakujeruhiwa.Tayari tumethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokeaTanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine wanne niWatanzania.Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni BiMwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla.Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikanahadi Alhamisi usiku wakati tukiandaa taarifa hii.Raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Bi Fatuma Mohammed Jama.Kuna taarifa ya mahujaji wanawake wawili ambao hadi Alhamisiusiku walikua hawajapatikana hivyo hatukua na uhakika juu ya usalama wao haditutakapowaona ama kupata taarifa zao. Ifahamike kuwa majina yamepatikana kupitia vitambulisho vyao
ambavyo wahanga wa tukio hili waliweza kuvichukua kutoka kwenye miili ya
marehemu.Nimepokea taarifa za majeruhi miongoni mwa mahujaji wetu waTanzania na baadhi ya majeruhi hao nimeonana nao mara baada ya kuruhusiwakutoka hospitalini.Vilevile nimeagiza maafisa wetu wa Bakwata nilionao hapa Minakuendelea kufuatilia habari na taarifa za mahujaji wetu katika hospitali na sehemuza kuhifadhia maiti. Nimefanya hivyo ili niweze kuwa na uhakika juu ya usalama wa
mahujaji wetu.Katika kipindi hiki cha taharuki kubwa tunafanya mawasiliano nawizara husika hapa Saudi Arabia kwa kushirikiana na serikali yetu kupitiaubalozi wetu hapa Saudi Arabia. Natambua uwepo wa mkanganyiko wa taarifa ambazo zinazidishataharuki kwa ndugu na jamaa wa mahujaji wetu. Nachukua fursa hii kuwaomba ndugu na jamaa wa mahujaji kuwa
watulivu na kuwa na subra katika wakati huu mgumu sana kwetu sote.Tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana na Insha Allah mara tutukipata taarifa za uhakika basi tutawafahamisha.Kutokana na idadi ya maiti kuwa kubwa serikali ya Saudi Arabiawanaendelea na zoezi la kutambua uraia wa kila mwili ili waweze kutoa taarifatunatarajia wakati wowote tutakuwa tumepata taarifa zaidi.Wabillahi Tawfiiq.Sheikh Abu Bakari ZuberiMufti wa Tanzania.MECCA, Saudi Arabia

0 comments:
Post a Comment