Meneja wa zamani wa Manchester
United Sir Alex Ferguson alitaka mshahara wake uongezwe maradufu baada
ya mshahara wa Wayne Rooney kuongezwa pakubwa 2010.
Rooney alikuwa ametishia kuhama United lakini mwishowe akatia saini mkataba wa kulipwa ujira wa £250,000 kila wiki.
"Niliwaambia
sikudhani ilikuwa haki kwa Rooney kulipwa mshahara mara mbili ya
mshahara wangu,” Ferguson amesema kwenye kitabu kipya.
"[mwenyekiti
mwenza wa United] Joel Glazer alisema: 'Nakubaliana nawe kabisa lakini
tufanye nini?’ Ilikuwa rahisi. Tuliamua hakuna mchezaji anayefaa kulipwa
mshahara mkubwa kunishinda.”
Kwenye kitabu chake kipya kuhusu
usimamizi chenye jina Leading , Ferguson anasimulia kuhusu kipindi cha
mpito alipoondoka Manchester United 2013 baada ya kuwa kwenye usukani
miaka 26, akisema: "Tungeliisimamia vyema.”
Raia huyo wa Scotland,
aliyeshinda mataji mawili ya Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya, mataji 13 ya
Ligi ya Premier, vikombe vitano vya FA na vikombe vinne vya League,
alirithiwa David Moyes, aliyefutwa miezi 10 baadaye.
Lakini
mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 73 anasema alitaka pia kuzungumza na
aliyekuwa kocha wa Barcelona ambaye sasa ananoa Bayern Munich Pep
Guardiola kabla yake kumteua Moyes.
Anasimulia pia jinsi meneja wa Chelsea Jose Mourinho, aliyekuwa
mkufunzi mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti, Jurgen Klopp wa Borussia
Dortmund na Louis van Gaal, ambaye ndiye mkufunzi wa sasa United,
walilengwa kumrithi.
"Nilimpenda [Pep] sana," Ferguson salisema
baada ya kukutana naye New York mwaka 2012. "Nilimuomba Pep anipigie
simu kabla yake kukubali ofa ya kujiunga na kilabu nyingine lakini
hakunipigia na alijiunga na Bayern Munich Julai 2013.
0 comments:
Post a Comment