Watetezi wa haki za binadamu wa Syria wamesema watu 38 wameuawa na wengine zaidi ya 150 wamejeruhiwa kufuatilia mashambulio ya waasi katika mji wa Alepo kaskazini mwa nchi
hiyo.
Mashambulio hayo yalifanywa vitongoji vinavyoshikiliwa na majeshi ya serikali katika mji
huo wa Aleppo uliogawanyika waasi wakishilikia upande wa mashariki na serikali upande wa
magharibi.
Taarifa za awali zilisema watu waliouawa walikuwa 20 na kwamba mashambulio hayo yalikuja siku moja baada ya mashambulio mengine mawili ya mabomu katika mji wa Hassakeh ambapo watu 20 waliuawa na wengine 40 kujeruhiwa.
Umoja wa Mataifa unakadiria zaidi ya watu 200,000 wamepoteza maisha na wengine milioni
11 wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa mgogoro wa Syria mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment