Image
Image

Jeshi la Burkina Faso litabaki madarakani hadi utakapofanyika uchaguzi.

Jeshi la Burkina Faso litabaki madarakani kufuatia mapinduzi yake ya wiki iliyopita hadi utakapofanyika uchaguzi ambao umesogezwa mbele kutoka tarehe 11 ya mwezi ujao kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali hadi tarehe 22 Novemba mwaka huu.
Msimamo huo umetolewa na kusisitizwa na kiongozi wa utawala wa kijeshi Jenerali GILBERT DIENDERE wakati wa mazungumzo yanayodhaminiwa na wapatanishi wa Afrika Magharibi.
Mwishoni mwa wiki mmoja wa wapatanishi Rais YAYI BONI wa Benin alizungumzia uwepo wa ufumbuzi wa mapinduzi hayo ambao chini yake serikali mpya ya mpito ingemrejesha rais wa mpito Bwana MICHEL KAFANDO aliyepinduliwa.
Kumekuwa na vurugu tangu kutokea kwa mapinduzi hayo Alhamisi iliyopita ambapo watu 10 wameuawa na jumuiya ya kimataifa kulaani mapinduzi hayo na Umoja wa Afrika kusimamisha uanachama wa nchi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment