Image
Image

Viongozi wa Ulaya wanajiandaa kuweka msukumo wa pamoja juu ya wimbi la wahamiaji barani Ulaya.

Maelfu zaidi ya wahamiaji wameingia Austria mwishoni mwa wiki wakati viongozi wa Ulaya wanajiandaa kuweka msukumo wa pamoja wa mwitikio wa wimbi la wahamiaji barani Ulaya.
Austria ilikuwa inatarajia kuwasili leo kwa wahamiaji zaidi wakati Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi nne za Ulaya Mashariki wanatarajia baadaye leo kuwa na mazungumzo ya mgogoro wa wahamiaji hao.
Katika wiki ya shughuli za kidiplomasia kukabiliana na mgogoro wa wahamiaji hao hapo kesho Mawaziri wa Ndani wa Umoja wa Ulaya nao watakutana kuzungumzia suala hilo na kufuatia keshokutwa kwa kikao kisichokuwa cha kawaida cha viongozi wa Umoja huo.
Rais FRANCOIS HOLLANDE wa Ufaransa amesema hakuna nchi mwanachama katika Umoja wa Ulaya itakayosamehewa kuchukua watu wenye haki ya hifadhi wakati Rais wa Baraza la Umoja huo Bwana DONALD TUSK amesema umoja huo usaidie kuboresha maisha ya wakimbizi wa Syria karibu na makwao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment