JK ahudhuria maziko ya Kanali mstaafu AYUBU SHOMARI KIMBAU.
Rais JAKAYA KIKWETE jana jioni ameungana na mamia ya waombolezaji katika maziko ya aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Mafia, Mkoa wa Pwani, kwa miaka mingi, Kanali mstaafu AYUBU SHOMARI KIMBAU.
Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya msikiti wa kijiji chao cha Baleni, Kilomita 21 kutoka Kilindoni, mji mkuu wa Wilaya ya Mafia.
Ndege iliyombeba Rais KIKWETE ilitua Uwanja wa ndege wa Kilindoni, saa 10 jioni akiongozana na Mama SALMA KIKWETE na Rais amekwenda moja kwa moja Baleni kwa maziko Mzee KIMBAU.
Maziko hayo yaliendeshwa kwa heshima na taratibu za Uislam na kijeshi kwa vile hayati KIMBAU alipata kuwa mwajiriwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Baada ya kutoka makaburini, Rais KIKWETE alikwenda kuipa pole familia ya marehemu iliyoko nyumbani kwa kaka yake marehemu.
Kanali mstaafu AYUBU SHOMARI KIMBAU alifariki dunia alfajiri ya juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment