Image
Image

JK akabidhiwa tuzo ya uongozi bora Afrika.

SIKU mbili baada ya kutunukiwa Nishani ya Amani na Utulivu katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Rais Jakaya Kikwete jana alikabidhiwa tuzo nyingine ya kimataifa, ya Utawala Bora barani Afrika kwa mwaka 2015.
Tuzo hiyo aliyokabidhiwa jana ilipokolewa kwa niaba yake na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro katika sherehe iliyofanyika Julai 25, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Rais Kikwete ametunukiwa tuzo hiyo na Bodi ya Uongozi ya Africa Archiever’s Award kwa kutambua mchango wake katika maeneo ya uongozi na utawala bora wakati wa uongozi wake wa miaka 10 wa Tanzania.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jana Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, Kaimu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Bahame Nyanduga.
Akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo, Waziri Migiro alisema kwa kupata tuzo hiyo, Rais Kikwete anaungana na viongozi wengine mashuhuri Afrika ambao wamepata tuzo hiyo wakiwemo Rais wa zamani wa Ghana, Hayati John Atta Mills, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma na Askofu Desmond Tutu, kiongozi wa Kanisa la Anglikana nchini Afrika Kusini ambaye pia ni mwanaharakati mashuhuri barani Afrika.
Alisema Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa Waafrika mashuhuri 1,202 ambao majina yao yalipendekezwa kwa ajili ya kutunukiwa tuzo hiyo kwa mwaka huu, lakini Bodi iliyomtunukia Rais Kikwete tuzo hiyo imeridhishwa zaidi na mchango wake mkubwa katika kujenga na kuleta utawala bora katika miaka yake 10 ya uongozi wake.
Katika hafla hiyo, Rais alisema hakuweza kwenda kupokea tuzo hiyo Afrika Kusini kwa sababu wakati huo alikuwa katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini Australia, lakini akaongeza kuwa amefurahi kutunukiwa tuzo hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment