Image
Image

JK:‘Nikistaafu sitalazimisha mtu kuniomba ushauri’.

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa kiongozi anapokuwa amemaliza muda wake wa uongozi na kustaafu, hawezi tena kuanza kudai kwa nini hasikilizwi na uongozi mpya na kwa nini kuomba ushauri.
Rais Kikwete aliyasema hayo usiku wa kuamkia Jumatano alipozungumza katika hafla ya kumuaga ambayo iliandaliwa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, mjini Dar es Salaam.
“Nilisikia mtu mmoja analalamika majuzi kuwa anahama chama kimoja kwenda kingine kwa sababu haombwi ushauri. Sasa wewe ulikwishakuwa Waziri Mkuu, umemaliza ngwe yako ya uongozi, unalazimisha kuombwa ushauri kwa nini?” Alieleza Rais Kikwete.
Aliongeza: “Mimi namaliza ngwe yangu ya uongozi. Nastaafu. Naondoka. Kama Rais anayekuja ataona ni jambo mwafaka kutaka ushauri, nitachangia kwa kadri ya uwezo wangu. Lakini kiongozi aliyestaafu hawezi kulazimisha kuombwa ushauri.
“Rais yeyote anakuwa amekamilika. Anao washauri wake. Kama ni kuhusu usalama mpo nyie wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vimekamilika. Mtampa ushauri Rais anayekuja kama mlivyokuwa mnanipa mie.”
Aidha, aliwaambia maofisa hao wa vyombo vya ulinzi na usalama: “Na wala siombi nyie mje kwangu kuomba ushauri kwangu. Nendeni kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wetu. Vinginevyo mtanitengenezea fitina na kiongozi wangu.
Sitalazimisha wala kulalamika kuwa sijaombwa ushauri.” Rais Kikwete anamaliza muhula wake wa pili kikatiba baadaye mwaka huu kumpisha Rais wa Awamu ya Tano.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment