Akizungumza
jijini Tanga wakati wa makabidhiano ya mashine hizo ndogo zenye uwezo
mkubwa kiutendaji,mjumbe wa shirika hilo Bibi,Zahra Nuru amesema lengo
ni kusaidia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na ile ya wilaya
ya Pangani ambapo wahisani wameelekeza kuwa akina mama
wajawazito wanapofika kwa ajili ya huduma hiyo wasitozwe fedha na kila
baada ya miezi sita wapewe taarifa zinazoonesha imesaidia akina mama
wangapi na walionusurika kifo baada ya kupta huduma ya mshine hizo.
Amesema
hatua hiyo inafuatia makundi ya akina mama kutokuwa na uwezo wa kulipia huduma
hiyo na hivyo kusababisha kati ya kina mama 100,000 wanaobeba ujauzito kila
mwaka kati yao 400 hufariki dunia kwa sababu ya matatizo mbali mbali ya
ujauzito na wakati wa kujifungua.
Kabla ya
kukabidhiwa mashine hizo,katibu tawala mkoa wa Tanga Bwana.Salum Chima
ameshukuru kwa msaada huo na kuwaagiza watendaji wa hospitali husika
kuhakikisha wanapata wataalam wenye uzoefu na matumizi yake ili kuepuka
matumizi mabaya yasiyoweza kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la
huduma zinazotolewa na mashine hizo.


0 comments:
Post a Comment