Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, akihutubia kwenye Mkutano huo wa Kampeni, uliofanyika kwenye
Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba
3, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, akizungumza na Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.
Mbunge aliemaliza muda wake wa Jimbo la Ole Zanzibar, Mh. Rajab Mbarouk akihutubia kwenye Mkutano huo.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha akizungumza na wananchi wa Mpanda.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.
Freeman Mbowe, akimkabidhi mfano wa funguo, Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Jonas
Kalinde, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Urais, uliofanyika Uwanja wa
Shule ya Msingi Kashaulili, Mpanda Mkoani Katavi leo Septemba 3, 2015.
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya
mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa,
amesema wanaompiga vita walie tu kwa sababu hawezi kuzuia mafuriko kwa
mkono.
Lowassa ametoa kauli hiyo mjini hapa jana, alipokuwa akihutubia
mkutano wa kampeni katika viwanja vya Kashaulili vilivyoko Mpanda,
mkoani Katavi. “Nilishasema siwezi kuzuia mafuriko haya kwa mkono, sasa
yanawasumbua wao, nasema siwezi kuyazuia kwa mkono,” alisema Lowassa
baada ya kupanda jukwaani na kushuhudia maelfu ya wananchi wa Mpanda
waliohudhuria mkutano wake.
Akizungumzia operesheni tokomeza iliyofanyika nchini mwaka jana na
kusababisha madhara kwa watu mbalimbali, Lowassa alisema kama
atafanikiwa kuingia madarakani, ataunda tume kuchunguza operesheni hiyo
ili kujua ni kwa nini Serikali haikuwalipa fidia waathirika.
“Mwaka jana Serikali iliunda Tume ya Operesheni Tokomeza, lakini
najua bado kuna malalamiko kwa baadhi ya wananchi. “Wakati wa operesheni
hiyo watu waliuawa, wapo waliofiwa, wengine walifilisiwa na hawakupewa
fidia kwa madhara waliyoyapata.
“Kwahiyo, Mungu akinijalia nikaingia madarakani, nitaunda tume
kuchunguza operesheni hiyo ili kujua ni kwanini wananchi hawakufidiwa.
“Vilevile najua kuna mgogoro wa shamba la Efatha na wananchi ambapo
wananchi wanasema ni shamba lao na mwekezaji huyo anasema ni mali yake.
“Kwahiyo, kama nitaingia madarakani, nitachunguza jambo hili kwa
sababu haiwezekani mgogoro huo uchukue miaka mitatu bila ufumbuzi wakati
mwenye mamlaka ya kuumaliza ni rais mwenyewe,” alisema Lowassa.
“Wawekezaji tunawahitaji, lakini lazima tuwalinde wakulima wadogo,
kwahiyo nitachunguza kuona haki iko wapi. “Pia tutaunda tume kuchunguza
mgogoro wa Bonde la Rukwa kwa sababu hatutaki migogoro ya wakulima na
wafugaji iendelee kuwapo,” alisema.
Mwaka jana, Serikali ilianzisha Operesheni Tokomeza iliyolenga
kukabiliana na uuaji wa wanyamapori wakiwamo faru na tembo uliokuwa
umekithiri nchini. Baada ya operesheni hiyo kuanzishwa, washiriki
waliendesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo baadhi ya
watu waliuawa, wengine walipata ulemavu wa kudumu na baadhi walipoteza
mali zao katika mazingira yasiyokubalika.
Kutokana na hali hiyo, Bunge liliiagiza Kamati ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembeli,
ichunguze jinsi operesheni hiyo ilivyotekelezwa.
Baada ya uchunguzi wa kamati hiyo na ripoti kuwasilishwa bungeni,
mawaziri wanne walitenguliwa uteuzi wao baada ya kuonekana walishindwa
kutimiza wajibu wao wakati wa operesheni hiyo.
Mawaziri hao ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis
Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk. Mathayo David.
MBOWE
Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia
mkutano huo, alisema safari yao ya kuingia madarakani, imerahisishwa na
Lowassa kwa kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono.
“Safari yetu ya mageuzi ilikuwa kama safari ya treni ya kutoka Dar es
Salaam kwenda Kigoma. Baada ya kumpata Lowassa, sasa safari yetu ni
nyepesi, lakini tunaomba Watanzania mtuunge mkono kwa sababu bado ina
vikwazo.
“Nyota ya uongozi kwa Lowassa ilikuwa ya miaka mingi ila CCM
hawakujua kama anapendwa na wananchi ndiyo maana wakampuuza, wakamkejeli
na kumsemea uongo.
“Kwahiyo, naomba wana mageuzi tusiwatukane walioko CCM kwani wapo watakaotusaidia kama ilivyo kwa Lowassa,” alisema Mbowe.
Pamoja na hayo, aliwasisitizia Watanzania umuhimu wa kuwachagua wagombea wote wa Ukawa ili wasaidie kuleta maendeleo nchini.
MGEJA
Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,
Khamis Mgeja, alisema ni aibu kwa Serikali ya CCM iliyokaa madarakani
kwa miaka 50, kuendelea kuomba misaada kutoka kwa wafadhili.
Pamoja na hayo, alisema CCM haina sababu ya kuendelea kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania kwa kuwa imejaa walarushwa.
“CCM imejaa wala rushwa na kutokana na mfumo huo, ndiyo maana
wanapokaa hawajadili masuala ya wananchi na badala yake wamekuwa
wakijadili masuala yao binafsi.
“Kuna wana CCM wamekuwa wakisema hawawezi kukihama chama chao, lakini
nawaambia CCM ni kama nyumba inayoungua na kinachotakiwa sasa ni wao
kuhama na kujiunga na Ukawa.
“Kwahiyo, nawaambia tena, mgombea wa CCM ndugu Magufuli hafai kuwa
rais wa nchi hii, kwani ni mbabe na ndiye amekuwa akivunja nyumba za
watu bila kuwalipa fidia,” alisema Mgeja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
















0 comments:
Post a Comment