Mkufunzi mkuu wa Chelsea Jose
Mourinho amesema anahisi jambo lisilo la kawaida,baada ya kilabu yake
kukumbana na mwanzo mbaya zaidi wa ligi kuu katika miaka 29.
Mabingwa
hao wa ligi ya Premier walilazwa na Everton Jumamosi, hiyo ikiwa mechi
yao ya tatu kushindwa katika mechi tano walizocheza msimu huu. Matokeo
hayo yamewaacha nambari 17 kwenye jedwali.
Vijana wa Mourinho
watakutana na Maccabi Tel Aviv ya Israel mechi ya hatua ya makundi
katika Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya Jumatano.
"Nawahakikishia kuwa niko salama," alisema. “Sina raha. Sijazoea kushindwa mara nyingi hivyo lakini sasa nazoea hali hii.”
Akaongeza:"Huwezi kunitarajia niseme kila kitu kiko shwari, na kwamba kuna
nicheko na mzaha. Watu wanapokosa ufanisi wanaopigania sana, basi
watavunjika moyo.
"Tunajua kwamba sisi ni – mabingwa wa Uingereza.
Mashabiki huimba hilo. Hakuna anayeweza kutupokonya ufanisi tuliopata
kufikia sasa au vikombe tulivyoshinda au historia yetu, unaweza kujaribu
lakini huwezi kufanikiwa.
"Unapozoea kushinda kila wakati, basi
unapokosa kushinda unahisi jambo lisilo la kawaida. Baadhi hukabiliana
na hali hii vyema, wengine hawawezi.”
Mourinho amesema hayo akihutubia wanahabari kuhusu mechi hiyo ya Jumatano dhidi ya Maccabi Tel Aviv.
0 comments:
Post a Comment