Serikali ya Madagascar imetangaza kuanzisha kampeni
ya kutoa chanjo ya ugonjwa wa kupooza kwa watoto
milioni 11.3 kote nchini.
Kampeni hiyo iliyoanza siku ya Jumatatu, inalenga kutoa chanjo
kwa watoto walio na umri wa kati ya miaka 0 – 15 kwa kipindi
cha siku tano nchini Madagascar.
Mkuu wa idara ya chanjo katika wizara ya afya ya Madagascar,
alisema kwamba wahudumu 22,171 wa kiafya watashiriki kwenye kampeni
hiyo na kutoa chanjo katika hospitali 3,177 kote nchini.
Kampeni hiyo iliyoanzishwa kwa msaada wa fedha dola milioni
4 kutoka kwa WHO, itawezesha watoto kupata chanjo
ya ugonjwa wa kupooza bure kwa siku tano.
Wizara ya Afya nchini humo imetangaza kuripotiwa kwa kesi 10 za
ugonjwa wa kupooza katika miezi 12 ya mwisho.
Ukosefu wa chanjo ni hatari kwa watoto kwa
kuwa unasababisha ugonjwa wa kupooza unaoweza kupelekea watoto
kuwa walemavu.
0 comments:
Post a Comment