Kundi kubwa la wahamiaji limekesha kwenye mpaka wa Hungary na Serbia katika juhudi za
mihangaiko ya kutafuta hifadhi katika nchi za Ulaya.
Hali hiyo imejitokeza baada ya Hungary kufunga lango lake lisilo rasmi lililopo mpakani
mwa nchi hizo mbili na hivyo kuwaacha wahamiaji wanaotaka kwenda kaskazini mwa Ulaya
kuwalazimu watafute njia nyingine mbadala .
Maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika mpakani mwa Hungary na Serbia kila siku kujaribu
kuingia barani Ulaya na wahamiaji wengi wameelezea masikitiko yao baada ya njia yao
kufungwa.
Vyombo vya habari vya Serbia vimesema mabasi ya wahamiaji sasa yamekuwa yanaelekezwa
Croatia ambako watapanga kuelekea Slovenia, Austria na hatimaye Ujerumani ambayo nayo
huenda ikapiga marufuku wahamiaji kupata baadhi ya mafao ya huduma za jamii.
0 comments:
Post a Comment