Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani ambapo amesema kuwa vifaa vingine vishaanza kusambazwa mikoani na zoezi la mwisho litakua ni kupeleka karatasi za kupigia kura huku utata wa majimbo akisema umekwisha tatuliwa.
Aidha Bw, Kailima pia alitolea ufafanuzi suala la jimboo la Lushoto ambalo Mgombea wake mmoja alifariki na kusema kuwa uchaguzi wa jimbo hilo utasogezwa mbele huku akitolea ufafanuzi zaidi wa kisheria juu ya mgombea yoyote anapofariki.
Kailima aliongeza kuwa kwa wale wanachuo ambao siku ya kupiga kura itawakuta tofauti na maeneo waliojiandikishia walitakiwa kuhakiki katika vituo walivyopo sasa ili waweze kupiga kura za wagombea wa nafasi zote katika eneo alililopo.
0 comments:
Post a Comment