Wanariadha wa Kenya walizidi kuonesha
umahiri wao katika mashindano ya 42 ya mbio za masafa marefu
yaliyoandaliwa siku ya Jumapili mjini Berlin nchini Ujerumani.
Mashindano hayo ya Berlin Marathon ya
mwaka huu yalijumuisha jumla ya wanariadha 41,224 kutoka nchi
127.
Kwa upande wa wanaume, mwanariadha Eliud Kipchoge kutoka Kenya
alimaliza wa kwanza mbio hizo kwa muda wa 2:04:01 huku Mkenya
mwenzie Eliud Kiptanui akifuatia kwa muda wa 2:05:22.
Feyisa Lilesa kutoka Ethiopia alimaliza wa tatu kwa muda wa 2:06:57.
Na kwa upande wa wanawake, mwanariadha wa Kenya Gladys
Cherono naye alishinda mbio hizo kwa muda wa 2:19:25
huku akifuatiwa na wanariadha wa Ethiopia Aberu Kebede
aliyemaliza wa pili kwa muda wa 2:20:48 na Meseret
Hailu aliyemaliza wa tatu kwa muda wa 2:24:33.
0 comments:
Post a Comment