Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon, alifanya mkutano
wa mazungumzo na rais wa Misri Abdulfattah al-Sisi nchini humo
Ban na Sisi walijadili masuala ya mchakato
wa amani katika kanda ya Mashariki ya Kati, na kuipongeza serikali ya Misri
kwa mchango wake kuhusiana na utatuzi wa mzozo wa Israel na Palestina.
Ban pia alidhihirisha furaha yake kwa hatua iliyochukuliwa
na Sisi ya kuwaachilia huru wafungwa 100 wakiwemo wanahabari
wa Al-Jazeera siku chache zilizopita nchini Misri.
Vile vile Ban alitoa wito wa uongozi bora kwa Sisi
na kumhimiza kuzingatia na kuheshimu haki za kibinadamu kama kiongozi kote
nchini Misri na katika kanda ya Mashariki ya Kati kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment