Image
Image

Mfalme wa Cambodia arudi nyumbani baada ya kufanyiwa matibabu mjini Beijing.


Mfalme Norodom Sihamoni wa Cambodia ameripotiwa kurudi nyumbani kwake siku ya Jumapili akiongozana na mamake ambaye ni Malkia wa zamani Norodom Monineat, baada ya kufanyiwa matibabu kwa kipindi cha mwezi mmoja mjini Beijing nchini China.
Familia hiyo ya kifalme ilipokewa na rais wa seneti Say Chhum, spika wa bunge Heng Samrin, mke wa Waziri Mkuu Bun Rany pamoja na balozi wa China nchini Cambodia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Phnom Penh.
Katika kipindi cha matibabu ya mwezi mmoja, Mfalme Sihamoni alikutana na rais wa China Xi Jinping alipohudhuria sherehe ya maadhimisho ya vita vya China na Japan iliyofanyika tarehe 3 Septemba.
Mfalme Sihamoni mwenye umri wa miaka 62 hufanyiwa ukaguzi wa kiafya na matibabu mjini Beijing nchini China mara moja kwa kila miezi sita.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment