Nchi ya Sierra Leone imeanza
tena upya kuhesabu siku 42 baada ya wagonjwa wawili wa mwisho wa Ebola
kutolewa katika kituo cha matibabu cha Mathene kilichoko mjini Makeni.
Shughuli hiyo ya kuhesabu siku 42
ilianzishwa tena upya siku ya Jumapili baada ya wakazi wa miji ya Kambia
na Bombali kukamilisha siku 21 za kutengwa kwenye karantini kufuatia
kuzuka kwa kesi mpya za Ebola.
Hapo awali, hesabu ya siku 42
iliyoanza mwezi mmoja uliopita ilivurugika baada ya mwanamke mmoja mwenye umri
wa miaka 67 kufariki kwa Ebola mjini Kambia, na mwanafunzi mmoja
wa kike mwenye umri wa miaka 16 kufariki mjini Bombali.
Wakati huo huo, kituo cha
kukabiliana na Ebola nchini humo kimetangaza zawadi ya fedha Leones
milioni 5 kwa mtu yeyote atakayetoa maelezo kuhusiana na Kadiautu Kamara
ambaye anashukiwa kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na mwanamke aliyefariki Kambia.
Kadiatu ameripotiwa kupotea siku 28 zilizopita kwa woga wa
kufanyiwa matibabu ya ugonjwa wa Ebola.
Kwa mujibu wa taratibu za afya, eneo
lolote linaweza kutangazwa kumaliza janga la Ebola iwapo hakutoonekana
kesi yoyote kwa muda wa siku 42.
0 comments:
Post a Comment