Meneja msaidizi wa kituo bw.saidi
sakala amedai tangu kituo kianzishwe mwaka (1993) hakijawahi kuwa na uzio jambo
ambalo limekua ni kikwazo kwao kutokana na vibaka wanaoingia mchana na usiku
kupora mali za kituo na hivi sasa wanapora hata nguo na viatu vya watoto na
kutishia kuwadhuru watoto wa jinsia ya kike.
Naye meneja wa NSSF mkoa wa
Shinyanga Bw.James Mashinga amesema NSSF kama shirika la hifadhi ya jamii lina
wajibu wa kuhakikisha makundi ya watu wenye uhitaji kama watoto wa kituo cha
imani wanasaidiwa ili kuboresha maisha yao huku akitoa mwito kwa mashirika
mengine ya binafsi na ya serikali kujenga utamaduni wa kusaidia makundi hayo
ili kuondoa hali ya unyonge na kujisikia kama binadamu wengine.
Nao baadhi ya watoto wanaishi
katika kituo hicho wamewataka wasamaria wema yakiwemomashirika ya serikali na
binafsi kuwasaidia kwa kutoa misaada ya chakula na mahitaji mengine kama
shirika la NSSF linavyofanya mara kwa mara hali itakayoondoa adha na wasiwasi
wanayopata kutokana na mazingira ya kituo chao.



0 comments:
Post a Comment