Kundi kubwa la watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za jadi,wameteka magari ya mizigo na magari madogo binafsi,kujeruhi vibaya watu waliyokuwemo kwenye magari hayo na kuwapora fedha, simu na vitu vingine.
Tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo katika Mji wa Ndanda Mkoani Mtwara ambapo watu hao waliweka kizuwizi cha magogo kati kati ya barabara ya Masasi -Lindi na kuzuia magari yote yaliyopita katika eneo hilo.
Mashuhuda walionusurika katika tukio hilo wamedai muda mfupi baada ya tukio walitoa taarifa Kituo cha Polisi Ndanda,Polisi Wilaya ya Masasi na Polisi Mkoa wa Mtwara lakini hawakufika katika tukio kwa muda muafaka japo majambazi hao walichukua zaidi ya saa moja na nusu wakiendelea na kitendo cha uporaji.
Dakika chache kabla ya Askari Polisi kufika katika eneo la tukio watu hao walitoweka na kusikika wakitamka tuondoke noma inakuja.
Home
News
Majambazi wakiwa na silaha za jadi wameteka magari ya mizigo na magari madogo kisha kujeruhi Mtwara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment