Sheikh
Abubakary Zubeiry amechaguliwa kuwa mufti wa Tanzania baada ya mpinzani wake
Sheikh Ali Mkoyogole kujitoa dakika za mwisho kabla ya kufanyika kwa uchaguzi
kwa madai kuwa anaridhika na utendaji wa Sheikh Zubeir ambaye awali alikuwa
kaimu mufti kufuatia kufariki kwa aliyekuwa mufti mkuu wa tanzania wa awamu ya
pili Sheikh Shaaban Issa Bin Simba Jully mwaka huu.
Muda
mfupi baada ya uteuzi huyo mufti Zubeiry alipata fursa ya kuzungumza na wajumbe
wa bakwata ambapo pamoja na mambo mengine amewataka waumini wa dini ya kiislamu
kuliombea taifa amani wakati linakabiliwa na changamoto ya uchaguzi mkuu ujao
huku akitoa wito kwa watanzania kushiriki mchakato huo kwa utulivu ili kuilinda
tunu ya amani na upendo ambayo tanzania imekuwa ikijivunia kwa muda mrefu.
Akitoa
salamu katika baraza hilo mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa
wamewataka viongozi wa dini ya kiislamu kuendelea kuhubiri na kufundisha
waumini mafunzo ya kiroho ili kudumisha amani ya nchi lakini pia wasisahahu
kusisitiza elimu dunia ili taifa na watu wake kuondokana na utegemezi.
Kwa
upande wao baadhi ya Masheikh ambao ni wajumbe wa baraza kuu la bakwata wametoa
maoni yao kuhusu mufti huyo huku pia wakizungumzia nafasi ya waislamu katika
uchaguzi mkuu ujao.
Uchaguzi wa mufti mkuu wa Tanzania awali
ulikuwa na wagombea wanne ambao ni mufti aliyechaguliwa na aliyejitoa pamoja na
masheikh wengine wawili ambao walienguliwa katika kinyang’anyiro hicho na baraza
la maulamaa nchini ambao ni Sheikh Hamis Abass Mtupa na Hasan Ibrahim Kiburwa.


0 comments:
Post a Comment