Image
Image

Polisi waionya UKAWA*Yaitaka ifanye kampeni za kistarabu la sivyo itawachukulia hatua za kisheria.

Polisi Mkoani Mtwara imevitahadharisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi - UKAWA-  kufanya kampeni za ustaarabu vinginevyo itawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria iwapo vitaendelea kuwa sehemu ya kuvuruga amani katika kampeni zao.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara,  HENRRY MWAIBAMBE baada ya Chama cha NCCR-Mageuzi  kuanzisha vurugu katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Mtwara Mjini baada ya  mgombea ubunge wa Chama cha Wananchi - CUF - MAFUTAH NACHUMA, kutambulishwa rasmi kugombea jimbo hilo.
Amesema chama hicho kilianzisha vurugu kwa madai mgombea wa NCCR-Mageuzi  ndiyo aliyestahili kutambulishwa na kugombea jimbo hilo hali iliyosababisha kuwapo kwa vurugu.
Kufuatia tukio hilo Polisi imesema haitavumilia vurugu za namna hiyo  kuendelea  na endapo vyama hivyo vitashindwa kuelewana hakuna sababu za kufanya mikutano itakayosababisha vurugu.
Hata hivyo Kamanda MWAIBAMBE amesema ukiondoa kasoro hiyo, kampeni kwa wagombea wengine wa ubunge na udiwani zinaendelea vizuri nakuwataka  wananchi kuwa sehemu ya kulinda amani ili zoezi hilo lipite kwa amani na utulivu.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment