Image
Image

Jaji mkuu wa Tanzania amesema utoaji wa huduma za mahakama unamapungufu.


Jaji mkuu wa Tanzania Othmani Chande amekiri bado kuna mapungufu katika utoaji huduma za mahakama ambapo utafiti unaonyesha kwa kipindi cha miaka 12 kati ya watu kumi waliotafuta huduma hizo mmoja kati yao amekumbana na vitendo vya rushwa huku akibainisha katika kipengele cha uendeshaji wa kesi mahakamani asilimia 48 ya wananchi walohojiwa wamesema wanaridhika  na 45 wakisema kesi zinachukua muda mrefu.

Jaji Chande anatoa takwimu hizo katika mkutano wa baraza kuu la mahakama ambapo amesema takwimu hizo zimetokana na utafiti uliofanywa na taasisi ya repoa kwenye mikoa 13 nchini na kuhusisha baadhi ya mahakama za ngazi zote na kuwahoji wananchi zaidi ya 2000 ambapo umebaini pia kati ya watu wote waliohojiwa asilimia 82 wameridhishwa na kiwango cha huduma na asilimia 16 hawakuridhishwa .

Aidha jaji huyo ameelezea hatua mbalimbali zilizochukuliwa kwa watumishi wasio waadilifu ambapo kwa mwaka 2014/15 pekee wafanyakazi 22 walishtakiwa kwenye tume ya maadili ambapo 21 kati yao walifukuzwa kazi kwa kutozingatia maadili.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wamesema iwapo wananchi hawaridhiki na utendaji wa baadhi ya watumishi wa mahakama wasisite kutroa taarifa kwani mahakama kama muhimili ina mifumo ya uendesha ambayo ina fanya kazi na tume ya maadili ya utumishi wa umma. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment