Mwanasiasa kijana machachari wa Afrika ya Kusini JULIUS MALEMA ametolewa bungeni baada ya kukataa kufuta kauli yake baada ya kumshutumu Makamu wa Rais wa nchi hiyo Bwana CYRIL RAMAPHOSA kuwa ni muuaji.Bwana MALEMA alibebwa juu juu na kutupwa nje ya bunge na walinzi wa usalama baada ya
kukata kwake kutoka nje kwa hiari na maafisa wamesema atasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa siku tano.
Mwezi uliopita Bwana MALEMA alimshutumu Bwana RAMAPHOSA kwa kuhusika kwake na mauaji ya mwaka 2012 ambapo watu wachimba migodi 34 waliokuwa wamegoma waliuawa na polisi kwa kupiga risasi.
Tume ya uchunguzi kuhusu mauaji hayo ilimsafisha Bwana RAMAPHOSA.


0 comments:
Post a Comment