Kikosi kimoja cha wanamgambo wanaounga mkono serikali ya Sudan kufanya mauaji ya halaiki,ubakaji na unyama kwa raia katika Jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo.
Katika ripoti yake Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema ukiukaji huo wa haki za binadamu umekuwa unafanywa na kikundi hicho kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.
Mgogoro wa jimbo la Darfur ulianza mwaka 2003 wakati raia wengi wasio wa makabila ya Kiarabu walipochukua silaha kukabiliana na manyanyaso waliyokuwa wanafanyiwa na serikali.
Maelfu kwa maelfu ya watu wameuawa na wengine wamekimbia makazi yao kutokana na machafuko ya Darfur.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment