Umoja wa Mataifa umedai kuwepo kwa ukiukaji wa haki za binadamu katika kuelekea uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Umesema kumekuwa matukio 24 yanayohusiana ukiukaji wa haki za binadamu mwezi uliopita yakiwemo ya ukamataji watu ovyo na vitisho ikilinganishwa na matukio 14 kama hayo mwezi uliotangulia wa Julai.
Hayo yameelezwa na Ofisi ya pamoja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ambapo Mkurugenzi wake Bwana JOSE MARIA ARANAZ amesema wasi was wa kisiasa umezidi kuongezeka katika kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika miezi 14 ijayo.
Katika uchaguzi huo Rais JOSEPH KABILA aliyeshika madaraka baada ya baba yake kuuawa mwaka 2001 anatakiwa na katiba kuachia ngazi lakini wapinzani wanamshutumu kwa kujaribu kuendelea kushika madaraka.
Home
Kimataifa
Umoja wa Mataifa umedai kuwepo kwa ukiukaji wa haki za binadamu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment