Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.Itakumbukwa kuwa tarehe 28 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa kuwa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano wakiwa wamefariki dunia.Majina ya baadhi ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-1. Abdul Iddi Hussein2. Awadh Saleh Magram3. Burhani Nzori Matata4. Yussuf Ismail Yusuf5. Saleh Mussa Said6. Adam Abdul Adam7. Archelaus Antory Rutayulungwa8. Farida Khatun Abdulghani9. Rashida Adam Abdul10. Hamida Ilyas Ibrahim11. Rehema Ausi Rubaga12. Faiza Ahmed Omar13. Khadija Abdulkhalik Said14. Shabinabanu Ismail Dinmohamed15. Salama Rajabu Mwamba16. Johari Mkesafiri Mwijage17. Alwiya Sharrif Salehe Abdallah18. Hafsa Sharrif Saleh AbdallahMbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa.Aidha, Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliokufa Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji unaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji wetu waliopotea.Vilevile, Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za Mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege wakati Mahujaji hao wakiingia nchini humo. Wizara inaamini kuwa taarifa za alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua Mahujaji wetu.Pamoja na jitihada zote hizo, Ubalozi pia unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo.Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Dar es Salaam29 Septemba, 2015
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment