TUME ya Taifa ya Uchaguzi NEC
imesema kuwa watu wote wenye ulemavu watapata nafasi ya kupiga kura kuchaguwa
Diwani,Mbunge na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na
kuwaandalia sehemu maalumu ya wao kupiga kura kwakuwa wanahaki za msingi kama
watu wengine tofauti na ilivyokuwa inaelezwa kuwa watu hao hawataweza kupiga
kura.
Kauli hiyo imetolewa hivi leo Jijini
Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya watu wenye ulemavu na NEC mkutano huo
wenye lengo la kuwapatia uelewa kuelekea uchaguzi mkuu.
Kuhusu malalamiko yatolewayo na
viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa juu ya mchakato mzima wa uchaguzi kwa
wengine kuona kama tume hiyo haitatenda haki kwenye uchaguzi wa mwaka huu Jaji Lubuva
amedai kuwa hakuna haja ya kuanza kulalamikia pasipo kuwa na sababu kwani tume
hiyo inajuwa wajibu wake na hivyo itatenda haki kwa kila mmoja kwa kuwa yenyewe
ndio yenye dhamana hadi dakika ya mwisho.
Hata hivyo Tume hiyo ya
uchaguzi imeendelea kusisitizia vyama vyote nya siasa kufuata maadili na kanuni
wakati wa kampeni zao kwani hakitasita kukichulia hatua kali chama ambacho
kitatumia mda mwingi jukwaani kuwasema watu badala ya kunadi sera zake.
Aidha Lubuva amesema kuwa
tiyari washaa vifikishia taarifa vyama vyote kufuata sheria ya uchaguzi ya
mwaka 2015 kwa kuacha kutumia mda mwingi kujadili watu,bali tumewataka
watangaze sera za chama husika na sio kutoa matusi jukwaani kwani kufanya hivyo
ni ukiukwaji wa sheria za uchaguzi kwakuwa wananchi wanataka sera si kuwasema
watu wengine ama kuwakejeli.
0 comments:
Post a Comment