Msafara wa mgombea urais
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa umepata wakati
mgumu hivi leo Muheza mkoani tanga baada ya wananchi kuzuia msafara wake kwa
muda kutaka asimame waongee naye kabla ya kufika sehemu anayo elekea kuhutubia.
Mh.Lowassa ambaye
alikuwa kwenye gari ya wazi aambalo anafanyia nalo mikutano yake huko jijini Tanga
ililazimu kusimama kuwasikiliza huku gari hilo likiwa limezungukwa na wananchi
hao ambao ni wapenda mabadiliko huku wakiimba nyimbo zenye imani na Mh.Lowassa
na kuahidi kuwa hawata muangusha Octoba 25 kwakuwa wanapenda mabadiliko.
Jana vilevile Mkutano wa
LOWASSA katika jiji la Tanga ulikumbana
na balaa la aina yake baada ya watu kadhaa kuzimia, huku wengine kujeruhiwa na
kisha mabomu kadhaa ya machozi kuvurumishwa na polisi kutawanya maelfu ya
wafuasi muda mfupi baada ya kumalizika.
Hali ya mkanganyiko
katika mkutano huo wa Lowassa, anayeungwa mkono pia na muungano wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NLD, NCCR-Mageuzi na Chama
cha Wananchi (CUF), ilianza kuonekana mapema wakati maelfu ya watu
walipojitokeza kwenye viwanja vya Tangamano.
Baadhi ya watu, hasa wanawake walijikuta
wakiwa hoi hoi kutokana na joto na kukosa hewa, hali iliyowalazimu wahudumiwa Msalaba
Mwekundu kuingilia kati na kutoa huduma ya kwanza kwani wengi wao walionekana
wakizimia na kuanguka chini.
Hata hivyo leo hii huko muheza wananchi kwa nyakati tofauti
wamekua wakisema kuwa wana imani ya asilimia 100 na Mh.LOWASSA kua akichaguliwa
kuwa rais wa Tanzania kilio chao cha kutapa tapa bila ajira kitapatiwa ufumbuzi
kwakuwa wanamuona ni mtu mwenye maamuzi magumu na mpenda mabadiliko.
Wananchi hao wamesema kuwa hawaoni sababu ya kila kukicha kilio kikubwa kwa
vijana ni ajira jambo ambalo limekuwa nijanga la taifa miaka nenda rudi,hadi
kusababisha vijana wengi kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na mambo
mengine,ambapo wamesema wanaendelea kusikiliza sera za kila mmoja wa wagombea
lakini kwa mwaka huu lazima wafanye mabadiliko ili waone ahadi zitolewazo bila
kutekelezeka je zitatekelezeka.
Baada ya muda nitakuletea ripoti kamili kutoka Muheza,Like
Page yetu na kuwa wa kwanza kusoma taarifa zetu.
0 comments:
Post a Comment