Image
Image

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Samba Panza asema uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utaahirishwa.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba Panza amesema uchaguzi mkuu nchini humo utaahirishwa kwa sababu za kiusalama.
Akizungumza kutoka New York alikokuwa akihudhuria mkutano mkuu wa viongozi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, kiongozi huyo pia amesema hataitikia shinikizo za kumtaka ajiuzulu.
Waandamanaji wamekuwa wakiitisha kujiuzulu kwake wakidai ameshindwa kukomesha mapigano.
Hayo yamejiri huku shirika la habari la Reuters likisema Bi Panza ameamua kurejea nyumbani mapema kufuatia kuzuka upya kwa mapigano Bangui.
Watu zaidi ya 30 wameuawa kwenye mapigano hayo na afisi za mashirika ya kutoa misaada kuvamiwa na kuporwa.
Wafuasi wa wanamgambo wa Kikristo wajulikanao kwa jina anti-Balaka walishambulia gereza siku ya Jumatatu, na kuwatorosha mamia ya wanajeshi na wanamgambo waliokuwa wamefungiwa humo.
Jamuhuri ya Afrika ya kati imekuwa ikikumbwa na machafuko tangu kundi la waasi wa Kiislamu la Seleka kuchukua madaraka mwezi Machi mwaka 2013.
Kundi la Seleka baadaye liliondolewa madarakani, hali iliyosababisha machafuko.
Maelfu ya watu waliyakimbia makazi yao. Kwa sasa taifa hilo linaongozwa na serikali ya mpito.
Uchaguzi mkuu ulikuwa umepangiwa kufanyika Oktoba, mwezi mmoja kabla ya Papa Francis kuzuru Bangui.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment