Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amedai mshambuliaji wake Diego Costa amekuwa akionewa na maafisa wasimamizi wa soka.
Akiongea
na wanahabari kuhusu mechi ya leo kati ya kilabu yake na Porto ya Ureno
katika Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya, Mourinho alisema kuna hamu kubwa ya
kumsimamisha au kumpiga marufuku mchezaji huyo miongoni mwa waamuzi.
Costa
alipigwa marufuku mechi tatu na Shirikisho la Soka la Uingereza baada
ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu wakati wa mechi dhidi ya
Arsenal ligi kuu.
Lakini yuko huru kucheza dhidi ya Porto leo kwani marufuku hiyo haigusi mechi za Ulaya.
Alipoulizwa
iwapo angelipenda kuwa na wachezaji 11 walio kama Costa uwanjani,
Mourinho alisema: “Tungeshindwa kila mechi, kwa sababu hamu ya kumpiga
marufuku iko juu mno kiasi kwamba tungekosa wachezaji wa kuanza nao
mechi.”
“Nina furaha tu kwamba kwa sasa nina mmoja tu na mwache acheze hadi waamue kumpiga marufuku tena.”
Costa amekosa mechi mbili Uingereza, na pia atakosa mechi ya wikendi dhidi ya Southampton.
Kwenye
kikao hicho na wanahabari, Mourinho pia alionya wachezaji wake kwamba
hakuna aliye salama iwapo kilabu hiyo itaendelea kuandikisha matokeo
mabaya.
Mourinho amekuwa akimuweka benchi John Terry mechi mbili
zilizopita za Ligi ya Premia, ihali Branislav Ivanovic na Cesc Fabregas
pia wamekosolewa kutokana na uchezaji wao.
"Watu wasioguswa, ni
uendelevu pekee unaoweza kukupa hadhi hiyo,” alisema Mourinho, ambaye
vijana wake wamo nambari 14 ligini baada ya mechi saba kucheza.
0 comments:
Post a Comment