Baraza la habari nchini kwa kushirikiana na BBC Media Action wametoa mafunzo ya namna ya kuandika habari za uchaguzi kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro.
Akifungua mafunzo hayo Ofisa program wa MCT, Tumbi Kiganja amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa maalum wakati huu ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini jinsi ya kuandika habari za uchaguzi mkuu.
Amesema katika kipindi hiki ni wajibu wa baraza hilo kutoa elimu ya namna ya kuandika habari za uchaguzi ili kuepusha migongano ya kimaslahi kati ya waandishi wa habari na wagombea wa vyama vya siasa.
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo, Fili Karashani amesema kuwa ni wajibu wa waandishi wa habari kuandika habari zote zinazotokea kwenye uwanja wa kampeni bila woga wala upendeleo ili mradi tu ziwe za kweli.
0 comments:
Post a Comment