Nahodha wa zamani wa Nigeria Daniel Amokachi
amejiuzulu wadhifa wake kama meneja wa kilabu ya ligi kuu ya Nigeria FC
IfeanyiUbah baada ya kuhudumu wiki tano pekee.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa awali
ameeleza hamu yake ya kutaka kushinda vikombe na kuhakikisha kilabu hiyo
inafana.
Lakini ameamua kuondoka baada ya msururu wa matokeo
mabaya na kutoelewana kati yake na mmiliki wa kilabu hiyo.
“Nasikitika kuondoka baada ya kipindi kifupi hivi
lakini kandanda inaendelea,” Amokachi ameambia BBC.
"Nilikuwa shabiki wa kilabu hii kabla ya
kuteuliwa kwangu kama meneja kwa sababu ya msingi uliopelekea kuundwa kwake.
"Lakini sasa naitakia kila la heri na
nitafuatilia hatua wanazopiga kwa fahari kuu.”
Ripoti zimedokeza kuwa Amokachi hakufurahishwa na
sera ya klabu hiyo ya kutumia barabara hatari usiku kurejea nyumbani baada ya
kucheza mechi za ugenini.
Msimamo wake ulimfanya kukosana na milionea
anayemiliki klabu hiyo, Ifeanyi Ubah.
Mfanyabiashara huyo anaaminika kuchukulia hatua ya
kocha huyo kuwa kukaidi mamlaka yake.
Amokachi alikataa kusema lolote alipoulizwa kuhusu
suala hilo.
“Soka haitabiriki na hakuna wakati wa kwenda mbele
na nyuma,” alisema.
"Imekuwa heshima kubwa kuhusika katika kilabu
hii lakini kwa sasa safari yangu imefikia kikomo FC IfeanyiUbah."
0 comments:
Post a Comment