Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlos Dunga
ametaja kikosi kitakachoanza kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali
za kombe la dunia za mwaka 2018 dhidi ya Chile pamoja na Venezuela mapema mwezi
ujao.
Dunga ametaja kikosi chake kwa kumuengua nahodha na
mshambuliaji wa mabingwa hao wa kihistoria duniani, Neymar da Silva Santos
Júnior kufuatia adhabu ya kufungiwa michezo minne iliyotolewa shirikisho la
soka la Amerika ya kusini CAMNEBOL wakati wa fainali za mataifa ya ukanda huo
zilizochezwa miezi mitau iliyopita.
Kikosi kamili kilichotajwa na Carlos Dunga tayari
kwa mpambano ya kuelekea nchini Urusi kusaka ubingwa wa dunia mwaka 2018,
upande wa makipa ni Jefferson (Botafogo), Marcelo Grohe (Grêmio) na Alisson
(Internacional)
Mabeki ni Rafinha (Bayern Munich), Marcelo (Real
Madrid), Filipe Luis (Atlético de Madrid), Fabinho (Monaco), David Luiz (PSG),
Miranda (Inter de Milão), Marquinhos (PSG), Gil (Corinthians)
Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho
(Manchester City), Elias (Corinthians), Renato Augusto (Corinthians), Lucas
Lima (Santos), Lucas Moura (PSG), Willian (Chelsea)
Washambuliaji: Douglas Costa (Bayern), Philippe
Coutinho (Liverpool), Oscar (Chelsea), Roberto Firmino (Liverpool), Hulk
(Zenit)
Brazil wataanza kupambana na Chile mjini Santiago
kwenye uwanja wa Nacional Julio Martínez Prádanos, oktoba 8 na kisha watarejea
nyumbani kuchezana Venezuela oktoba 13 kwenye uwanja wa Castelão, uliopo mjini
Fortaleza.
0 comments:
Post a Comment