Mgombea mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia
chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ),Mh.Juma Duni Haji amesema kwamba
iwapo,watanzania watamchagua mgombea urais wa chama hicho Mh.Edward Lowassa
kuongoza serikali ya awamu ya tano, atahakikisha wachimbaji wadogo wadogo wa
madini katika mkoa ya Geita wanatengewa maeneo rasmi pamoja na kufufua mazao
makuu ya biashara ikiwemo Pamba na Tumbaku ili kuiwezesha serikali kuendelea
kupata fedha nyingi za kigeni katika soko la dunia.
Akihutubia mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu ambazo zimefanyika
katika majimbo ya Bukombe na Busanda mkoani Geita kwa nyakati tofauti,na
kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi hasa katika mji mdogo wa Katoro,mgombea
mwenza huyo wa Chadema Mh.Juma Duni haji,maarufu kama ‘Mjela Jela’amesema kuwa
baadhi ya ahadi zilizotolewa na rais Jakaya Kikwete mwaka 2010 wakati akinadi
ilani ya chama cha mapinduzi hazijawahi kutekelezwa hadi sasa anapomaliza muda
wake wa uongozi,huku akiwataka watanzania kupima ahadi zinazoendelea kutolewa
na mgombea urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli kama zina tija,vinginevyo hawana
budi kufanya mabadiliko kwa kumchagua Mh.Edward Lowassa.Bofya Kuona zaidi->>http://bit.ly/1gwMPm4
0 comments:
Post a Comment