Madereva mkoani Ruvuma wametakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuzuilika.
Ajali hizozimeelezwa kuwa zimekuwa zikipoteza maisha ya watu wengi na wengine kuachwa na ulemavu wa kudumu mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,CHANDE BAKARY NALICHO ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bwana SAIDI MWAMBUNGU katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabani Mkoa wa Ruvuma, ISSA LUTAVI amesema mwaka jana ajali zilisababisha vifo 92 na majeruhi 531.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment