Image
Image

TFDA- yapiga marufuku matumizi ya vipodozi visivyo na kiwango kwa wananfunzi nchini Tanzania.

Mamlaka ya Chakula na Dawa - TFDA-  imepiga marufuku matumizi ya vipodozi visivyo na kiwango kwa wananfunzi wanaosoma katika shule mbalimbali nchini kwa kuwa vimekuwa vikichangia wanafunzi wengi  kupata magonjwa ya ngozi na kujiingiza katika vishawishi.
Akizungumza na wamafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari Mkoani Kagera alipokuwa  akitoa elimu juu ya madhara ya vipodozi vinavyoingizwa nchini kwa njia za magendo kutoka nchi mbalimbali duniani, Mkaguzi  wa Dawa na Vipodozi Kanda ya Ziwa,  VENAS BURUSHI amesema vipodozi hivyo vimekuwa na madhara makubwa katika jamii na hasa kwa wasichana wenye umri mdogo.
Katika hatua nyingine Makaguzi  Mkuu wa Dawa na vipodozi amebainisha matatizo  mbalimbali ambayo mara nyingi yanachangia  kuingizwa  vipodozi hivyo kwa njiia zisizo halali kuwa ni pamoja na baadhi ya watumishi wa TFDA kurubuniwa na wafanyabiahsara wa vipodozi .
Nao baadhi ya wanfunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Hekima wameipongeza Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi kwa kutoa elimu hiyo muhimu na kwamba watakuwa mfano wa kuigwa katika jamii .

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment