Wamesema ni ngumu kuendelea kumuamini Slaa kwa alicho kizungumza
kwa kumtupia Shutuma Edward Lowassa jambo walilosema endapo kungekuwa na
utofauti angesimama na kusema tokea awali lakini sio muda huu wa kampeni.
Jana Dk. Slaa alisema Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, siyo mwadilifu kwakuwa ana tuhuma mbalimbali.
Alisema kiongozi huyo ana kashfa mbalimbali ikiwamo kupokonya ardhi na kujimilikisha.
Akimzungumzia Lowassa, alisema: “Ni dhambi kupotosha watu, unahalalisha uovu kwa masilahi yako binafsi, dhambi haihalalishwi na dhambi, CCM hawana ujasiri wa kukemea dhambi, Lowassa alipofika ni kwa sababu ya CCM.
“Tumeng’ang’ania mambo ya Richmond, mimi na Lowassa tuna ugomvi, tangu 2008 nilimwambia acha kulalamika, nikamwambia sema Richmond ni ya nani? Leo anatoka anasema alishinikizwa na mkubwa, ni nani huyo?”
Alisema ripoti ya Bunge dhidi ya Richmond, ilionyesha namna suala hilo lilivyoanza tangu Serikali ya awamu ya tatu hadi zabuni ilivyotangazwa na mzabuni kupatikana.
“Baadaye miezi mitatu baada ya mzabuni kupatikana, Lowassa aliandika barua akieleza hofu yake juu ya Richmond na namna vyombo vya habari vinavyoripoti,” alisema.
Pamoja na barua hiyo, Dk. Slaa alihoji kwanini Lowassa aliiandika kwa wakati huo na kwanini mzabuni alitakiwa kupatikana ndani ya siku 10 badala ya 40.
“Chadema ilikuwa ni tumaini jipya, lililojengeka kwahiyo vijana wengi wakisikia jina la Chadema wanajitokeza, sitaki vijana wangu mfike baadaye muanze kujilaumu kama mwaka 2010 mlivyoambiwa maisha bora kwa kila Mtanzania.
“Tulihamasika baada ya kuambiwa maisha bora, matokeo yake tukajikwaa kwa sababu ya maneno mazuri kwenye tisheti, 2005, sukari ilikuwa 500 leo sh ngapi? Mnayajua.
“Juzi Mwakyembe (Dk. Harison, aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza Richmond) kasema kesi ya jinai haina mwisho, itaamka wakati wowote,” alisema.
Alisema baada ya mkutano wake wa jana, baadhi ya watu watasema ameichana Chadema na kuitetea CCM, lakini imebidi iwe hivyo kwa sababu ndiyo ukweli.
“Niko tayari kushusha heshima yangu hata dunia nzima ili kuridhisha nafsi yangu,” alisema.



0 comments:
Post a Comment