Image
Image

Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya wanawake ya Uganda kutoshiriki mashindano ya All Africa Games 2015 kutokana na matatizo ya kifedha.


Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya wanawake ya Uganda, imetangaza kutoshiri mashindano ya All Africa Games 2015 yatakayofanyika nchini Congo kutokana matatizo ya kifedha.
Katibu msaidizi wa kamati ya michezo kitaifa Nicholas Muramagi, alitoa maelezo siku ya Jumanne na kutangaza kutoshiriki kwa timu ya taifa ya mpira wa kikapu inayojumuisha wanadada 15 kwenye mashindano hayo.
Muramagi aliarifu kuchukuliwa kwa hatua hiyo kutokana na uchache wa fedha zilizotolewa na serikali ya Uganda.
Timu ya taifa ya Uganda ilifuzu kushiriki mashindano ya All Africa Games 2015 baada ya kufanya vyema katika mashindano ya kikanda ya kundi la 5 yaliyoandaliwa mjini Kampala.
Baada ya kukosa mashindano ya All Africa Games 2015, sasa Uganda italazimika kusubiri mashindano ya AfroBasket Women 2015 yatakayoandaliwa kuanzia Septemba 24 hadi Oktoba 4 nchini Cameroon.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment